
Articles
-
4 days ago |
dw.com | Rashid Chilumba
Hayo yameelezwa na waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo Andrii Sybiha katika wakati viongozi wa mataifa manne ya Ulaya wako mjini Kyiv kwa ziara ya kuonesha mshikamano na taifa hilo lililo vitani. "Ukraine na washirika wake wako tayari kusimamisha mapigano bila masharti yoyote, kwa maana ya ardhini, angani na baharini kwa muda wa siku 30 kuanzia Jumatatu", ameandika waziri Sybiha kupitia mtandao wa kijamii wa X.
-
1 week ago |
dw.com | Rashid Chilumba
Merz, mwanasiasa wa kihafidhina kutoka muungano wa vyama ndugu vya CDU/CSU amekula kiapo cha kuwa kansela wa 10 wa Ujerumani jana jioni baada ya kuidhinishwa na bunge la taifa, Bundestag. Halfa fupi ya kupokea hati ya kuchaguliwa kwake na Bunge ilifanyika mjini Berlin kwenye makaazi ya Rais wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier na baadae Merz alikula kiapo mbele ya wabunge. Kuapishwa kwake kulifanyika baada ya siku ndefu na ya fedheha kwa Merz.
-
1 week ago |
dw.com | Rashid Chilumba
07.05.20257 Mei 2025Mwanasiasa wa kihafidhina Friedrich Merz ameapishwa jana jioni kuwa Kansela mpya wa Ujerumani. https://p.dw.com/p/4u1f6Amechukua wadhifa huo saa kadhaa baada ya kushindwa kupata wingi wa kura katika uchaguzi wa awali uliofanyika ndani ya bunge majira ya asubuhi. Kwenye kura ya pili, Merz alichaguliwa kwa kura 325 katika bunge hilo la taifa, Bundestag, lenye viti 630.
-
1 week ago |
dw.com | Rashid Chilumba
MigogoroAsia07.05.20257 Mei 2025India imefyetua makombora kadhaa ndani ya ardhi ya Pakistan mapema leo alfajiri na kusababisha vifo vya watu 8, katika mashambulizi yanayoweza kuzusha vita baina ya nchi hizo mbili jirani na hasimu wa miaka mingi. https://p.dw.com/p/4u1f5Mamlaka za Pakistan zimesema makombora ya India yalililenga jimbo linalozozaniwa na pande hizo mbili la Kashmir pamoja na mkoa wa mashariki wa Punjab.
-
1 week ago |
dw.com | Rashid Chilumba
07.05.20257 Mei 2025Baraza Maalumu la Siri kwa ajili ya kumchagua kiongozi mpya wa kanisa katoliki duniani, litaanza baadaye leo kwenye Makao Makuu ya Kanisa Katoliki mjini Vatican. https://p.dw.com/p/4u1f4Makadinali 133 kutoka kila pembe ya dunia watakusanyika kwenye kanisa dogo la Sistine kuanza zoezi la upigaji kura ili kumchagua mrithi wa Papa Francis aliyeaga dunia mnamo Aprili 21.
Try JournoFinder For Free
Search and contact over 1M+ journalist profiles, browse 100M+ articles, and unlock powerful PR tools.
Start Your 7-Day Free Trial →